Kwa mujibu wa taarifa ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, maandamano haya makubwa yalifanyika sambamba na mgomo wa kitaifa nchini Italia ulioitishwa ili kulaani mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala wa Kizayuni huko Ghaza. Italia imepangwa kuwa mwenyeji wa timu ya Israel tarehe 14 Oktoba katika mji wa Udine. Hata hivyo, UEFA, kwa mujibu wa ombi la wanachama wengi, imeweka kwenye ajenda yake kusimamishwa kwa timu ya Israel.
Waandamanaji wa Kiitaliano walikusanyika kwa utulivu na bila vurugu kwenye uwanja wa mpira, wakitoa kauli mbiu kama:
“Acheni tuuzuie Uzayuni kwa njia ya Muqawama .” “Mnawezaje kucheza mpira na Israel ambayo ni nchi ya kihalifu?”
Aidha, siku ya Ijumaa pia wafanyakazi na wanafunzi wengi walifanya maandamano katika nchi mbalimbali kulaani kukamatwa na kufukuzwa kwa wanachama wa meli zilizobeba misaada ya kibinadamu kuelekea Ghaza.
Chanzo: Al Jazeera
Maoni yako